Kwa ajili ya kupunguza usumbufu: Gari za Atabatu Abbasiyya zinasaidia kupeleka wanafunzi katika vituo vya mitihani.

Maoni katika picha
Miongoni mwa misaada ya kibinadamu ni kupeleka wanafunzi kwenye vituo vya mitihani kwa ajili ya kuwaondolea usumbufu, hasa wale wanao ishi mbali na vituo vya kufanyia mitihani, na kuwawezesha kufika mapema katika vituo hivyo, kitengo cha magari ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa viongozi wake kimejitolea kubeba wanafunzi kutoka majumbani kwao hadi katika vituo vya kufanyia mitihani, kwenda na kurudi.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo kiongozi mkuu wa kitengo cha magari Ustadh Maitham Abdul-Amiir: “Sio mara ya kwanza, kitengo cha magari ya Atabatu Abbasiyya kimekua kikifanya hivyo siku za nyuma pia, hasa katika kusaidia wanafunzi wanao ishi mbali na vituo vya mitihani, tumeandaa gari kubwa zenye uwezo wa kubeba watu (50) na ndogo zenye uwezo wa kubeba watu (25)”.

Akaongeza kua: “Tumewasiliana na wazazi pamoja na idara za shule kuhusu swala hili, pia tukakubaliana sehemu ambazo ni rahisi wanafunsi kufika kwa aili ya kupanda gari kwa kuwapeleka na kuwarudisha, tumeanza kazi hii tangu siku iliyo anza mitihani na tutaendelea hadi siku ya mwisho”.

Wanafunzi na wazazi wameshukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake kwa kuwapa huduma ya usafiri na kuwawezesha kufika kwenye vituo vya mitihani kwa wakati na kurudi nyumbani mapema bila usumbufu wowote wa usafiri wala tabu ya joto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: