Adhuhuri ya Alkhamisi (23 Shawwal 1440h) sawa na (27 Juni 2019m) miongoni mwa ratiba ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya nne, yamefunguliwa maonyesho ya vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na picha na mabango ya kuchorwa matukio tofauti ya vita, maonyesho hayo yanafanyika katika eneo lililo pauliwa ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kamba ya uzinduzi imekatwa na jopo la viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wakiongozwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar.
Kuhusu maonyesho hayo tumeongea na msimamizi wake Ustadh Abbasi Radhwi amesema: “Washiriki wa maonyesho haya ni kituo cha Dirasaat Afriqiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wataalamu wa kiiraq wakiwa na mbao arubaini za michoro, pamoja na taasisi ya Anaamil Alhadhwaarah kutoka Baabil kikiwa na kazi arubaini na nane za aina tofauti”.
Akaongeza kua: “Miongoni wa walioshiriki pia ni kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kilicho kua na picha za aina mbalimbali, na idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambacho kilikua na makumi ya mabango”.
Akasema kua: “Maonyesho yatafanyika kwa siku mbili na yatapambwa na kazi za Sanaa mubashara, kama vile kuchora na kuandika kwa hati mbalimbali za kiarabu”.
Fahamu kua maonyesho haya ni moja ya ratiba za kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda linalo fanyika hivi sasa.