Kiongozi wa maahadi ya Qur’ani tukufu: Mwitikio wa wanafunzi katika mradi wa semina za Qur’ani unatusukuma kuongeza juhudi ya kuwahudumia na kuwafundisha.

Maoni katika picha
Mkuu wa maahadi ya Qur’ani tukufu Shekh Jawadi Nasrawi amesema kua: “Watumishi wote wa Maahadi wanafanya kila wawezalo katika kuwahudumia wanafunzi wanaoshiriki katika mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto (kiangazi), kinacho wasukuma zaidi ni mwitikio mkubwa wa wanafunzi katika masomo haya, pamoja na mapenzi ya kupata fursa ya kutumikia vizito viwili Qur’ani tukufu na kizazi kitakatifu (a.s)”.

Ameyasema hayo Shekh Nasrawi alipo tembelea vikao vya usomaji wa Qur’ani vinavyo endeshwa na tawi la Maahadi hiyo katika mkoa wa Najafu, vilivyo enea kila sehemu ya mji, akafafanua kua: “Mwaka huu tumepokea zaidi ya wanafunzi (22000) kutoka Karbala na mikoa mingine, nayo ni fursa kubwa ya kujifunza Dini tukufu kupitia Qur’ani na masomo mengine yanayo tokana na Qur’ani au Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), pia yanawajenga kiroho na kuwafanya kuwa watu wema maishani mwao”.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu imekua ikiendesha mradi huu kwa miaka mingi sasa, na inapata maendeleo makubwa mwaka baada ya mwaka katika kila sekta, ikiwa ni mapoja na kuandaa semina za wanafunzi na za walimu, pamoja na kufika katika miji mipya tuliyokua hatujaweza kuingia miaka ya nyuma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: