Vipande vya marumaru zinazo tolewa katika kuta na sakafu ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) vinaenda wapi?

Maoni katika picha
Mazuwaru na watu wanaofuatilia ujenzi unao fanyika katika haram ya Atabatu Abbasiyya wanajiuliza vinako pelekwa vipande vya marumaru zinazo tolewa katika sakafu na kuta za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa ajili ya kujibu swali hili na kuwaridhisha wale wanaotaka kujua hatima ya mabaki hayo tumekwenda kuongea na kitengo kinacho husika na kutunza mabaki hayo ambayo yanathamani kubwa, kitengo hicho kina miaka mingi tangu kianze kusimamia swala hilo, nacho ni kitengo cha zawadi na nadhiri idara ya marumaru, tumeongea na kiongozi wa idara hiyo Ustadh Maitham Rajaaq Ni’mah, amesema kua: “Zaidi ya muongo mmoja na nusu tangu ujenzi ulipo anza katika Atabatu Abbasiyya tukufu tulipata wazo la kunufaika na vipande vya marumaru vinavyo tolewa kwa ajili ya ujenzi na kuvitumia kwa tabaruku, huwa tunavitunza vizuri na kuwapa watu wanaokuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kua: “Utowaji wa marumaru hizo hupitia hatua tofauti na mwisho utengenezwa vizuri kitaalamu, hukusanywa na kuoshwa kisha huwekwa nakshi na maandishi chini ya watalamu walio bobea katika kazi hiyo kwa kutumia (cnc) halafu hukatwa katika viwango tofauti kama mawe ya vito na mikufu”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Hakika vipande hivyo hupewa zaairu kwa lengo la tabaruku, pesa ndogo ambayo hutolewa na mazuwaru kwa ajili ya vipande hivyo hutumika katika ujenzi wa maeneo ya ndani ya Ataba tukufu, na baadhi hutolewa bure kwa mazuwaru watukufu na wageni wa Ataba”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: