Atabatu Abbasiyya tukufu yazipa mkono wa pole familia za mashahidi wa Spaika

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu yazipa mkono wa pole familia za mashahidi wa Spaika, kwenye hafla ya kufunga kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda iliyo fanyika Alasiri ya Ijumaa (24 Shawwal 1440h) sawa na (28 Juni 2019m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Takrima hiyo inatokana na namna Atabatu Abbasiyya inavyo zijali familia za mashahidi wa Iraq zilizo jitolea baba, watoto na ndugu zao kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matakatifu kutokana na magaidi wa Daish waliokua wanafanya ufisadi (uharibufu) katika ardhi, hususan familia za mashahidi wa Spaika walio umiza roho ya kila muiraq, kutokana na unyama wa kuuwawa vijana zaidi ya (1700) wa Iraq wasiokua na hatia, walio uwawa kinyama na magaidi wa Daesh.

Kwa upande wao wanafamilia wa mashahidi wa Spaika wameushukuru uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwakumbuka, wakasema jambo hilo sio geni, Atabatu Abbasiyya imekua mstari wa mbele katika kusaidia familia za mashahidi sambamba na kuwajulia hali zao kila baada ya muda.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua na bado inaendelea kutoa misaada kwa familia za mashahidi walio itika wito wa Marjaa Dini mkuu wa kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: