Kufunga pazia la kongamano la kuadhimisha fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya nne.

Maoni katika picha
Baada ya siku mbili zilizo jaa ratiba ya vikao za mada za kitafiti na visomo vya Qur’ani na mashairi sambamba na maonyesho ya vitu mbalimbali vya Sanaa, Alasiri ya Ijumaa (24 Shawwal 1440h) sawa na (28 Juni 2019m) limefungwa kongamano la kuadhimisha fatwa tukufu ya kujilinda, kupitia hafla iliyokua na mahudhurio makubwa ya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Iraq.

Hafla ya kufunga kongamano imefanika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar, pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na idadi kubwa ya familia za mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi, kisha ukafuata usomaji wa maazimio ya kongamano na Dokta Riyadh Amidi kutoka katika kituo cha Al-Ameed Duwaliyyu Lidirasaat Walbuhuuth.

Halafu akapanda mimbari kijana Ali Hussein Kaadhim mmoja wa walionusurika katika mauwaji wa Spaika, akasimulia kisa cha kunusurika kwake na kifo, mambo aliyo pitia katika kujinusuru pamoja na mateso waliyo pata marafiki zake walio uwawa katika mauwaji hayo ya halaiki, kisha familia za mashahidi wa Spaika zikapewa mkono wa pole.

Mwisho kabisa wakapewa zawadi washindi wa mashindano yaliyo fanywa katika ratiba ya kongamano, sambamba na watafiti walioshiriki kuwasilisha mada na waandishi wa habari waliosaidia kutangaza matukio ya kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: