Dhulma haiwezi kuondolewa na muda.. Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlis ya kuomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s) kwa watumishi wake

Maoni katika picha
Katika kuomboleza kifo cha nuru ya sita miongoni mwa nuru za Muhammadiyya Imamu Jafari Swadiq (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kwa watumishi wake ndani ya ukumbi wa utawala, asubuhi ya Jumamosi (25 Shawwal 1440h) sawa na (29 Juni 2019m) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la watumishi na mazuwaru.

Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha Sayyid Ahmadi Twawiri Jawi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya akazungumza, katika mada yake aliongea vipengele vingi kuhusu maisha wa Imamu Swadiq (a.s), pamoja na mambo mengine ikiwemo elimu yake (a.s), na mazingira aliyoishi yaliyo muwezesha kwa kiasi fulani kutoa mafundisho ya Ahlulbait (a.s), na namna alivyo weza kuendelea kufundisha Dini baada ya baba yake Imamu Baaqir (a.s), katika kipindi cha Uimamu wake uliodumu miaka thelathini na nne, aliweza kutoa wanachuoni wengi waliofuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s), alifanikiwa kulinda na kufundisha madhehebu ya Ahlulbait (a.s).

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma kaswida zilizo amsha hisia za huzuni kutokana na msiba huo unao umiza umma wa kiislamu, baada ya kufariki kwake (a.s), huzuni ilienea kila sehemu na sauti za vilio ilisikika sana katika nyumba za bani Hashim pamoja na nyumba zingine, waislamu wakafurika katika nyumba ya Imamu wakiwa na majonzi makubwa kwa kuondokewa na mtu aliyekua anategemewa na waislamu wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: