Masayyid ambao ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaomboleza kifo cha babu yao Imamu Jafari Swadiq (a.s), aliye uwawa siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Shawwal, kwa kufanya majlisi za kuomboleza ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kuhusu maombolezo haya; kiongozi wa masayyid watumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Hashim Shami ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: (Miongoni mwa mambo yanayo fanywa na idara yetu ni kuhuisha matukio ya kidini, kuomboleza matukio ya misiba likiwemo hili la kifo cha Imamu Swadiq (a.s), tumefanya majlisi ya kuomboleza na ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ukafuata muhadhara ulio tolewa na Sayyid Mudhwaru Kazwini kutoka kitengo cha Dini, ameongelea vipengele vingi, alianza na kueleza historia kwa ufupi kuhusu maisha ya Imamu wa sita, na mambo makuu yaliyo tokea katika maisha yake kielimu, hadi kuuwawa kwake na Mansuur Dawaniqi, majlisi ikahitimishwa kwa kaswida iliyo taja tukio la kifo chake).
Majlisi ilikua na mwitikio mkubwa, imehudhuriwa na watumishi wengi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).