Wanaahidi kufuata nyayo zake: Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanampa pole Imamu wao Hussein katika kuomboleza kifo cha mjukuu wake Swadiq (a.s)

Maoni katika picha
Kutokana na kauli ya huyu tunayemkumbuka Imamu Jafari Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu.. Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu), kama kawaida yao katika kuhuisha matukio ya huzuni, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wametoa pole kwa Imamu Hussein katika kuomboleza kifo cha mjukuu wake Swadiq (a.s).

Watumishi watukufu walisimama kwa mistari wakiongozwa na katibu wao mkuu pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na kufanya matembezi ya kuomboleza ya pamoja baada ya Adhuhuri siku ya Jumamosi (25 Shawwal 1440h) sawa na (29 Juni 2019m), matembezi hayo yalianzia ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), walianza kwa kufanya majlisi ya kuomboleza kisha wakatembea kuelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) wakipitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Huku wakiimba kaswida za kuomboleza kutokana na msiba mkubwa uliotokea katika umma wa waislamu na watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika siku kama ya leo mwaka wa (148h) wakamuahidi kufuata nyayo zake katika kumhudumia babu yake na Ammi yake (a.s) pamoja na mazuwaru wao.

Walipo walisi katika haram tukufu ya bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s) wakapokewa na maukibu ya watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, wakafanya majlisi ya pamoja ndani ya ukumbi wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), na wakaimba kaswida za maombolezo zilizo taja utukufu wa Imamu Swadiq (a.s) na athari kubwa aliyoacha katika umma wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: