Maukibu ya kuomboleza: Watu wa Karbala wanaomboleza kifo cha Imamu Swadiq mbele ya kaburi la mjukuu wake Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s) kilicho umiza roho za watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) katika siku kama leo mwaka (148h), watu wa Karbala wamefanya matembezi ya kuomboleza katika mji wa Mash-had mbele ya kaburi la mjukuu wake Imamu Ali Ridhwa (a.s), pamoja na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na mazuwaru wa kiiraq waliopo huko, kwa ajili ya kuomboleza msiba ulioumiza waumini kote duniani.

Matembezi hayo yamefanyika siku ya Jumamosi (25 Shawwal 1440h) sawa na (29 Juni 2019m), chini ya usimamizi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa mawasiliano na uangalizi wa Atabatu Radhawiyya tukufu kwa ajili ya kuonyesha sehemu ya kuanzia na kumaliza matembezi ya watu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: