Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel yawaita watu wote waliojiandikisha katika program ya mafunzo wafike katika hafla ya ufunguzi.

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa wito kwa watu wote waliojiandikisha kwenye program ya mafunzo ya kujenga uwezo (PDC) wahudhurie wao pamoja na wazazi wao katika hafla ya ufunguzi wa masomo hayo itakayo fanyika Ijumaa ijayo tarehe (1 Dhul-qaada 1440h) sawa na (5 Julai 2019m).

Wakutane mbele ya jengo la Imamu Askariy (a.s) –hoteli ya Dallah ya zamani- iliyopo eneo la mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad) saa tisa Alasiri, hapo kutakua na magari ya kuwabeba wageni watukufu na watu wote waliosajiliwa katika program hiyo kwa ajili ya kuwapeleka sehemu itakapo fanyika hafla hiyo, ambayo inatarajiwa kufanyika katika jengo la Shekh Kulaini, ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye barabara ya (Bagdad – Karbala).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: