Msafara wa Alwafaa wagawa maji baridi ya kunywa kwa wanafunzi wa darasa la sita katika mji wa Mosul

Maoni katika picha
Katika kusaidia mazingira ya malezi na masomo kwenye mkoa wa Nainawa, msafara wa Alwafaa tawi la Mosul chini ya kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) kimegawa maji baridi ya kunywa kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya wizara ya kuhitimu darasa la sita.

Siku ya kwanza waligawa maji kwa wanafunzi (800) wavulana na wasichana pamoja na walimu wao, fahamu kua mitihani inafanywa katika majira ya kiangazi yenye joto kali, jambo hili linafanywa kwa mwaka wa pili mfululizo, wasimamizi wa ratiba hiyo wamesema kua wataongeza idadi zaidi katika siku zijazo hadi siku ya kumaliza mitihani, wakawatakia wanafunzi mtuhani mwema wenye mafanikio hususan baada ya kukomboa mji wao kutoka kwa magaidi wa Daesh na kuurudisha katika himaya ya taifa letu kipenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: