Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaimarisha ulinzi na usalama wa barabara zinazo tumiwa na mahujaji wa Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kinatoa huduma kwao

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) kimetangaza kua kimeimarisha ulinzi na usalama katika barabara zitakazo tumiwa na mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kinatoa huduma kwao.

Makamo katibu mkuu wa Ayabatu Abbasiyya na kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi Shekh Maitham Zaidi amesema kua: “Kikosi cha Abbasi (a.s) kitasambaza askari wake wa hakiba katika barabara ya Arúr inayo elekea katika nyumba takatifu sambamba na kuongeza siraha za kivita pamoja na ndege zisizokua na rubani”.

Akabainisha kua: “Maandalizi yote yanafanywa kwa kushirikiana na jeshi la serikali”.

Akaongeza kua: “Tutatoa huduma kwa mahujaji kupitia maukibu ya kikosi cha Abbasi pamoja na kuandaa mji wa mahujaji uliokua unatumiwa na wanajeshi wa serikali”.

Akasema: “Tutafanya mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni kwa ajili ya kueleza ratiba ya kikosi kuhusu swala hili”.

Fahamu kua kikosi cha Abbasi (a.s) tangu kuanzishwa kwake miaka mitano iliyo pita kimekua kikishiriki kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usamala katika barabara zinazo tumiwa na Mahujai, huteua baadhi ya askari wake pamoja na vifaa kwa ajili ya jambo hilo sambamba na kushiriki kwenye vita ya kukomboa taifa katika miaka ya nyuma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: