Sayyid Hussein Halo kiongozi wa kituoa cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu ya Atabatu Abbasiyya ametangaza kukamilika kwa maandalizi ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa awamu ya tano, kila kinacho hitajika kwa ajili ya mradi huo kimeandaliwa, kuanzia wakufunzi, vifaa na mahala pamoja na kuandaa ratiba za masomo tofauti.
Akaongeza kua: “Tayali tumesha pokea wanafunzi (60) kutoka mikoa tofauti ya Iraq wakiwemo watoto wa mashahidi na mujahidina kupitia kitengo cha Quráni tukufu katika Hashdi Shaábi”.
Akafafanua kua: “Selebasi ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa haijajikita katika usomaji wa Quráni peke yake, masomo ya malezi, aqida na fiqhi yamepewa umuhimu pia”.
Kumbuka kua huu ni mradi muhimu wa Quráni unao simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unaendeshwa na walimu wenye uwezo mkubwa kutoka ndani na nje ya Iraq, unalenga kuandaa kizazi cha wasomi wa Quráni, kupitia kuendeleza watoto wenye vipaji vya kusoma Quráni kwa muda mfupi, kwani mradi huu unalenga wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kwa kutumia kipindi cha likizo za kiangazi ambacho huwa ni miezi miwili takriban kuwafundisha mambo mengi kuhusu usomaji wa Quráni tukufu.