Kitengo cha Dini kinashiriki kutoa mafunzo kwenye semina za mahujaji

Maoni katika picha
Baada ya kufaulu mitihani waliyo pewa iliyo wapa kibali cha kuwa waongozaji wa kidini katika misafara ya hijja, kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki kutoa mafunzo kwenye semina za hijja na umra zinazo endelea katika mkoa wa Karbala kwa mahujaji watarajiwa wa mwaka huu.

Shekh Haidari Aaridhwi kutoka kitengo cha Dini ni mmoja wa wakufunzi wa semina hii, amesema kua: “Kutokana na kukaribia msimu wa hujja na mahujaji kuanza kujiandaa kwa safari hiyo, idara ya maelekezo na utafiti chini ya kamati ya hijja na umra kupitia tawi lake la Karbala, inafanya semina mbalimbali kwa ajili ya kuwafundisha ibada ya hijja wanaotarajia kwenda hijja, chini ya ratiba maalum yenye mihadhara (12) kwa kila msafara (kikundi) cha mahujaji, wanafundisha kwa nadhariya na vitendo, mafunzo hayo yataendelea hadi katika nyumba takatifu, kwani yanahusu mambo mengi ya aina tofauti, yanalenga kuwafundisha mambo yote yanayo husiana na hijj a kwa kiasi wataweza kuhiji kwa usahihi kabisa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: