Mchepuo wa uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed unafuata mfumo bora wa elimu na kukidhi viwango vya kisekula

Maoni katika picha
Sawa na michepuo (vitivo) vingine vilivyo chini ya chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, mchepuo wa uuguzi umepiga hatua kubwa katika kufikia ubora wa viwango vya elimu, miongoni mwa maendeleo yake ni kufanikiwa kuingia katika baraza la kuboresha viwango vya uuguzi katika vyuo vikuu vya serikali ya Iraq na vya binafsi.

Hivi karibuni baraza hilo limewakutanisha wawakilishi wa vyuo vingi vya uuguzi vya hapa Iraq, kwa ajili ya kufuatilia na kujadili utekelezaji wa majukumu ya rais wa wajumbe wa baraza hilo katika uboreshaji wa viwango vya vyuo vya uuguzi vya Iraq, kwa kiwango cha kimataifa kinacho fatwa na vyuo vikuu vikubwa duniani kote.

Mkuu wa mchepuo wa uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Naji Yasiri Almiyahi ameongea kuhusu mkutano huo kua: “Tumefanya jitihada ya kuwasiliana na vitivo vya uuguzi katika vyuo vikuu vya serikali na binafsi, kwa lengo la kukiingiza chuo chetu katika baraza la kuboresha viwango vya elimu ya vyuo vya uuguzi vya Iraq, tumejitahidi kukitangaza chuo kikuu cha Al-Ameed na kufadhili harakati mbalimbali za kielimu ikiwa ni pamoja na kuendesha vikao, makongamano na nadwa, leo tumefanikiwa kuwa wenyeji wa mkutano huu muhimu wa kujadili hali ya elimu na utendaji katika vyuo vya uuguzi pamoja na kujadili namna ya kuviboresha, sambamba na kuweka mikakati ya kupambana na changamoto za vyuo hivyo”.

Akabainisha kua: “Wajumbe wamejadili vigezo vinavyo tumiwa na baraza la kuboresha viwango vya elimu na wakakubaliana kufanya warsha kwa ajili ya kuviandika, pamoja na kujadili mapendekezo ya wizara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: