Ufumbuzi wa changamoto mbalimbali watolewa na kituo cha utamaduni wa familia kwa wakina mama

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea kutekeleza ratiba ya semina elekezi kwa wakina mama wa mkoa wa Karbala, wakiangazia matatizo tofauti ya kijamii na kuyatafutia ufumbuzi, chini ya wakufunzi mahiri wanao chambua (dadavua) kwa undani mazingira halisi ya jamii, kwenye darasa la kila wiki la wakina mama, darasa la mwisho katika ratiba hiyo liliangazia mambo makuu mawili, kwanza: (Mbinu za kuwasiliana na watoto), pili: (Mbinu za kupambana na changamoto za maisha).

Kiongozi wa kituo hicho Ustadhat Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), bado tunaendelea na ratiba yetu inayo lenga kujenga uwelewa kwa wakina mama kuhusu namna ya kuamiliana na watoto na mbinu za kuwasiliana nao kutokana na umri wao pamoja na jinsia zao, sambamba na kuangalia mambo mengine yanayo husiana na watoto, ikiwa ni pamoja na kupambana na changamoto za maisha pamoja na athari yake kwa familia, wakati wa kujadili mambo hayo mawili makuu, yameongelewa mambo mengi ya kimaisha na kutolewa mifano halisi mbalimbali, na kutaja utatuzi wa changamoto hizo”.

Akaongeza kua: “Washiriki walipewa nafasi ya kuuliza maswali ambayo yalijibiwa kisasa na kitaalamu zaidi”.

Akasisitiza kua: “Kuna mwitikio mkubwa unaotupa hamasa ya kuendelea na jambo hili, kwani mahudhurio yamekua yakiongezeka kila siku hii inatokana na kuridhishwa kwao na mada zinazo fundishwa”.

Fahamu kua harakati hii inasimamiwa na jopo la wataalam walio bobea katika mambo ya kifamilia na wana uwezo mkubwa wa kupambana na tatizo lolote katika sekta hiyo na kulipatia ufumbuzi.

Kumbuka kua kituo kinatoa wito kwa kila anayetaka kushiriki katika mradi huu apige simu namba (07828884555) au kwa kutumia mitandao wa mawasiliano ya kijamii (Viber, Whatsapp, Telegram) au ajiunge kupitia linki ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1 fahamu kua usafiri wa kwenda na kurudi umeandaliwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: