Shule za Al-Ameed zaanzisha ratiba ya (mtoto mbunifu)

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuwajenga watoto kimaadili na kuwafanya watumie vizuri kipindi cha likizo, shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya zinaendesha ratiba ya masomo na michezo waliyo ipa jina la (mtoto mbunifu).

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa ratiba hiyo Ustadhat Hadili Amuri amesema kua: “Ratiba hii itafanyika kwa siku (40), tunafundisha kupitia michezo, tunakusudia kuhakikisha watoto wanafaidika na kipindi cha likizo za majira ya kiangazi, na kuwafanya wasimalize muda kwa michezo isiyokua na faida kwao”.

Akafafanua kua: “Watoto tunao wakusudia wana umri wa kati ya miaka (4 / 6), mara nyingi hawakumbukwi kuwekewa ratiba yeyote ya ziada, hivyo hii ni ratiba pekee kwao”.

Akabainisha kua: “Ratiba inahusisha vitu vingi, kuna ratiba za michezo ya kuogelea kila siku, wanafundishwa kompyuta, pamoja na kuwafundisha mambo mbalimbali kwa vikundi utaratibu unao itwa (pembeni ya mwezi) unao husisha michezo ya watoto kwa vikundi pamoja na kuwafundisha mambo tofauti kupitia michezo hiyo, pia kuna kazi za mikono kama vile kuchora, kutengeneza maumbo kwa kutumia karatasi na vitu vingine vingi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: