Juhudi kubwa zimefanywa na idara ya haram tukufu katika kuweka marumaru mpya ndani ya ukumbi wa haram ya Abbasi

Maoni katika picha
Idara ya haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya juhudi kubwa wakati wa kazi ya kuweka marumaru mpya ndani ya ukumbi wa haram, imeshiriki kikamilifu kuandaa mazingira, imefanya kazi nyingi katika kufanikisha uwekaji wa marumaru.

Kiongozi wa idara ya haram tukufu bwana Haadi Hanuun ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu kazi hizo kua: “Watumishi wa idara yetu walifanya kazi ya kutandua mazulia, ukumbi wa haram waliugawa sehemu tano, walitandua mazulia kwa awamu katika kila sehemu, na baada ya kutanduliwa yalikua yanapelekwa kuoshwa katika kituo maalum cha kuosha mazulia ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akasema: “Baada ya kumaliza kazi ya kuweka marumaru, watumishi wetu wamerudi kutandika upya mazulia, ambapo walianza kusafisha na kupiga deki kisha ndio wakatandika mazulia”.

Fahamu kua ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi umewekwa marumaru mpya, baada ya marumaru za zamani kudumu zaidi ya nusu karne, mara ya mwisho kuwekwa marumaru ilikua katika miaka ya sabini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: