Ugeni wa waandishi wa habari watembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Ugeni wa waandishi wa habari wapatao (15) kutoka taasisi tofauti za vyombo vya habari, wakiongozwa na kiongozi wa idara ya habari ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Ali Khabbaaz wametembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya.

Miongoni mwa miradi waliyo tembelea ni Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji, wametembea katika korido zake na kuangalia mitambo na utendaki wa kazi unavyo endelea, wamefurahishwa sana na mitambo ya kisasa inayo tumika kutoka Ujerumani, pamoja na uzalishaji wa karatasi zenye viwango bora kabisa vya kimataifa, kisha wakaenda kutembelea hospitali ya rufaa Alkafeel wakasikiliza ufafanuzi wa kina kutoka kwa idara ya habari ya hospitali kuhusu namna wanavyo toa huduma za uuguzi.

Rais wa ugeni huo Ustadh Raadhi Mutarafi ambaye pia ni mkuu wa wahariri wa jarida la Haraak na katibu mkuu wa umoja wa waandishi wa habari wa Iraq amesema kua: “Tulipo kua tunaangalia mitambo ya uchapishaji ya Alkafeel tumeona miradi mikubwa na tulifurahi sana tulipo ona chapa ya msahafu wa kwanza kuchapishwa hapa Iraq, hili peke yake ni mafanikio makubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kua: “Kuhuzi ziara yetu katika hospitali ya rufaa Alkafeel tumeona vifaa tiba vya kisasa pamoja na wagonjwa wengi, hiyo ni dalili kua hospitali inatoa huduma nzuri, tunashukuru Atabatu Abbasiyya kwa kufanya miradi kama hii, nimatumaini yetu kua inamiradi ya kibiashara, kilimo na viwanda pia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: