Maoni katika picha
Kuhusu mradi huu tumeongea na kiongozi wa mradi wa mashine za kutotoa mayai za Alkafeel Mhandisi Dhiyaa Sharifi amesema kua: “Mradi huu ulianziswa mwaka (2016) kwa kushirikiana na watalam kutoka ulaya pamoja na watalam wa hapa nchini, nao unatumia mitambo bora na ya kisasa zaidi”.
Mmoja wa wasimamizi wa mashine za kutotolesha mayai Ustadh Abbasi Fadhili amesema kua: “Tunasambaza vifaranga katika mikoa yote ya Iraq kutokana na uwezo mkubwa wa mashine hizi katika kutotolesha mayai, kwani ni mashine za kisasa kabisa na vifaa vyake huagizwa kutoka Ulaya”.