Kituo cha utamaduni wa familia kimeendesha ratiba ya (kujenda uwezo) kwa wafanyakazi wa vitengo vya idara za malezi katika mkoa mtukufu wa Karbala

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimehitimisha mafunzo ya (kujenga uwezo), washiriki wa mafunzo hayo ni kamati ya maendeleo ya wanawake katika idara za malezi za Karbala.

Masomo hayo yalikua ya siku tatu mfululizo, mada mbalimbali zimewasilishwa, miongoni mwa mada hizo ni: (Namna ya kukabiliana na changamoto za kinasfi), (Misingi ya kufanikiwa uhusiano wa wanandoa), (Tiba kwa njia ya chakula na kupunguza uzito), pia kukawa na muhadhara kuhusu (Mbini za kuamiliana na watu), mwisho wa ratiba washiriki walikwenda kutembea katika jengo la Al-Afaaf la kibiashara kisha wakaenda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kumzuru mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s).

Bi Asmahani Ibrahim mkuu wa kituo hicho amesema kua: “Lengo la masomo haya ni kupunguza uzito kwa wanawake, kwani tabaka hili linahitaji kuwezeshwa kupambana na changamoto za kazini na nyumbani pamoja na watoto, wanahitaji pia kufahamu mabadiliko yanayo tokea kila siku, kituo kinatilia umuhimu mkubwa swala hili na siku zijazo masomo haya yatahusisha kundi kubwa zaidi la wafanyakazi kutoka sekta tofauti”.

Unaweza kuwasiliana na kituo kwa simu namba: (07828884555) pia namba hiyo imeonganishwa na (Viber, Whatsap na Telegram) hali kadhalika unaweza kujiunga kupitia linki ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: