Mwezi mosi Dhulqaada: Dunia imeangaziwa na nuru ya kuzaliwa kwa Fatuma Maasumah (a.s)

Maoni katika picha
Tunapokea mwezi wa Dhulqaada kwa kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa tawi tukufu miongoni mwa matawi ya mtu wa baraka, mwezi mosi Dhlqaada ni siku aliyo zaliwa bibi Fatuma bint wa Imamu Mussa Alkadhim mototo wa Imamu Jafari Swadiq (a.s) anayejulikana kwa jina la Maasumah.

Bibi Maasumah alizaliwa mwezi mosi Dhulqaada mwaka wa 183h katika mji wa Madina, akalelewa chini ya usimamizi wa kaka yake Imamu Ridhwa (a.s), kwa sababu Haruna Abbasiy alimuweka gerezani baba yake Imamu Mussa bun Jafari (a.s) katika mwaka alio zaliwa, kisha akamuua kwa sumu mwaka wa 183h, kwa hiyo akalelewa na ndugu zake chini ya usimamizi wa kaka yake Imamu Ridhwa (a.s).

Imepokewa kua kaka yake Imamu Ridhwa (a.s) ndiye aliye mpa jina la laqabu la “Maasumah”, pia imepokewa kua babu yake Imamu Swadiq (a.s) alimpa jina la “Karimat Ahlulbait” kabla ya kuzaliwa kwake, alikua binti bora zaidi katika mabinti wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s), kaburi lake lipo katika mji mtukufu wa Qum, ni kiburudisho cha macho ya watu wa Qum na watu kutoka kila sehemu husafiri kwenda kumzuru (a.s).

Kuna riwaya nyingi zinazo zungumzia utumufu wa kumzuru bi Maasumah (a.s), miongoni mwa riwaya hizo ni:

  • 1- Kutoka kwa Saádi bun Saidi, kutoka kwa Abu Hassan Ridhwa (a.s) anasema: Nilimuuliza kuhusu kaburi la Fatuma bint Mussa bun Jafari (a.s) akasema: (Atakaemzuru atalipwa pepo).
  • 2- Imamu Aljawaad (a.s) anasema: (Atakaezuru kaburi la shangazi yangu katika mji wa Qum atalipwa pepo).
  • 3- Kutoka kwa Saádi, kutoka kwa Imamu Ridhwa (a.s) anasema: (Ewe Sa’adi mnakaburi letu) nikamwambia: kaburi la Fatuma bint Mussa? Akasema: (Ndio, Atakaemzuru huku anatambua haki yake ataingia peponi).
  • 4- Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu anaharam katika mji wa Maka, na Mtume (s.a.w.w) anaharam katika mji wa Madina, na kiongozi wa waumini (a.s) anaharam katika mji wa Kufa, na sisi tuna haram katika mji wa Qum, atazikwa katika mji huo mwanamke katika watoto wetu anaitwa Fatuma, atakaemzuru ataingia peponi).

Mmoja wa washairi anasema:

Ewe binti wa Mussa na mototo wa watakasifu, dada wa Ridhwa na kipenzi wa Jabbaar.

Ewe thamani kubwa kutoka katika bahari ya elimu, Mwenyezi Mungu amekutukuza na kukuinua.

Wewe ni zawadi ya Imamu Ali kwa viumbe, fahari ya ukarimu ewe mwenye siri.

Ewe binti wa uongofu utaendelea kua mtakasifu, katika kila jambo lisiloridhiwa na Mwenyezi Mungu.

Atakaezuru kaburi lako malipo yake ni peponi, imepokewa hivyo katika riwaya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: