Hospitali ya Alkafeel: Tumefaulu kwa asilimia %100 katika upasuai wa (scoliosis)

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa mafanikio ya hospitali ya rufaa Alkafeel katika kufanya upasuaji wa aina mbalimbali, uongozi umetangaza kua kiwango cha mafanikio ni asilimia %100 katika upasuaji wa (scoliosis) tatizo hilo husababisha ulemavu kwa kiasi kikubwa.

Daktari bingwa wa upasuaji huo bwana Waaili Qassim amesema kua: “Tumefanya upasuaji huo kwa urahisi mkubwa sawa na inavyo fanyika katika hospitali kubwa za kimataifa, hii inatokana na kuwepo kwa vifaa tiba vya kisasa pamoja na madaktari mahiri wenye uzowefu mkubwa wa upasuaji huu”.

Akabainisha kua: “Upasuaji umefanikiwa kwa kiwango cha (%100) kiwango hicho ni zaidi ya vizuri kwa viwango vya kihospitali, kiwango cha tatizo kwa kila mgonjwa kilikua kati ya asilimia (%100) hadi (%70) kwa ujumla wakonjwa wote walio fanyiwa upasuaji wakubwa kwa wadogo matibabu yao yalifanikiwa”.

Akafafanua kua: Huu ni miongoni mwa upasuaji unao hitaji umakini wa hali ya juu, mgonjwa anaweza kuangalia kinacho endelea mbele yake huku akiwa amesimama kwa miguu yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: