Marjaa Dini mkuu katika khutuba la swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (1 Dhulqaada 1440h) sawa na (5 Julai 2019m), chini ya Uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai amezungumza vipengele vingi vya kimaadili vinavyo endana na mazingira halisi ya maisha ya sasa, jambo kubwa ametahadharisha matumizi ya dawa za kulevya, na miongoni mwa aliyo sema ni:
- - Kuna mambo yanatishia maadili ya jamii na kuishi kwa amani.
- - Matumizi ya dawa za kulevya yanaongezeka kwa kasi katika jamii.
- - Utumiaji wa dawa za kulevya unaenea kwa kiwango kikubwa katika tabaka la vijana wakike na wakiume na kuharibu mustakbali wao pamoja na uwezo wa akili na afya.
- - Yatupasa kua makini na jambo hili ambalo limeanza kuenea kwa vijana.
- - Kuna njia mbalimbali zinatumika kushawishi vijana wajiingine katika matumizi ya dawa za kulevya.
- - Hakuna njia imara za kuwalinda vijana na ushawishi huo.
- - Kuna umuhimu mkubwa wa kutafuta ufumbuzi wa haraka ili kuwakinga vijana wasidumbukie kwenye hatari ya matumizi ya dawa za kulevya.
- - Vyombo husika wanatakiwa kulipa umuhimu zaidi swala la kuzuwia biashara ya dawa za kulevya.
- - Tunahitaji kuundwa sheria itakayo ambatana na adhabu kali kwa wafanya biashara za dawa za kulevya.
- - Kuna udhaifu wa sheria na wala haziogopeshi wahalifu.
- - Watu wengi wanafanya biashara ya dawa za kulevya kwa ajili ya kutafuta utajiri wa haraka.
- - Lazima kuwe na sheria kali itakayo waogopesha wahalifu.
- - Baadhi ya wafanya biashara wa dawa za kulevya wanauhusiano wa karibu na viongozi wakubwa (vigogo) wa serikali wanao wasaidia kukwepa sheria.
- - Ukosefu wa ajira na kukaa bila shughuli yeyote ni miongoni mwa sababu zinazo wasukuma vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.
- - Kitu muhimu kwa kila mtu ni kujenga uwelewa katika jamii kuhusu madhara ya dawa za kulevya kuanzia kwenye familia, shule na maeneo mengine.
- - Watu wengi katika jamii hawayapi umuhimu unaotakiwa mambo ya malezi na kupambana na mmomonyoko wa maadili.
- - Mambo ya kisiasa yanapewa umuhimu mkubwa kushinda mambo ya kimalezi na maadili.
- - Mambo ya usalama yanapewa umuhimu mkubwa na hilo ni jambo zuri lakini haifai kusahau malezi na kusimamia maadili mema katika jamii.
- - Tunapo acha kutilia umuhimu malezi na maadili katika jamii hutokea matatizo mengi.
- - Uislamu uanatutaka kila kitu tukipe umuhimu unaostahiki.
- - Jamii zilizo endelea hukipa kila kitu umuhimu kinaostahiki.
- - Familia hujali sana kumsimamia mototo katika masomo ya sekula lakini zinasahau kumsimamia katika malezi na misingi ya maadili mema.
- - Jambo hilo limesababisha kutokea kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii.
- - Tunatakiwa kila kitu tukipe umuhimu kinaostahiki.
- - Sasa hivi tunatatizo kubwa la kuenea kwa utumiaji wa dawa za kulevya.
- - Kwa kiwango ambacho familia zinajali na kuthamini masomo ya sekula kwa watoto wao zinatakiwa zijali na kuthamini pia malezi ya kiroho na maadili mema.
- - Kuna baadhi ya vyombo vya habari vinatangaza mambo yasiyokua na maadili.
- - Tuna vijana wenye uwezo mzuri, ambao tunahitaji kunufaika na uwezo wao kama jamii hivyo lazima idara za shule na vyuo ziwe makini nao.
- - Tunatahadharisha kuanza kuenea kwa vituo vya uovu tena kwa majina mazuri hasa katika mji mkuu wa Bagdad.
- - Tunaviomba vyombo vya serikali vinavyo husika vifuatilie vituo hivyo na kuviweka chini ya uangalizi maalum kwani nje vinamajina mazuri wakati ndani vimejaa uovu na vinaharibu jamii.