Katika kupanda mbegu ya maarifa ya Quráni na tabia za kiislamu ndani ya nafsi za mabinti: Maahadi ya Quráni kitengo cha wanawake yaanza kutoa mafunzo ya msimu wa likizo za kiangazi

Maoni katika picha
Kufuatia kuanza kwa likizo za kiangazi pamoja na semina za Quráni zinazo simamiwa na Maahadi ya Quráni tukufu upande wa wavulana, Maahadi ya Quráni upande wa wasichana chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu mwaka wa nane mfululizo imekua ikiendesha semina za Quráni katika kipindi cha majira ya kiangazi kwa mabinti, kwenye matawi yote ya Maahadi yaliyopo (Bagdad, Waasit, Baabil, Dhiqaar, Karbala, Basra, Diwaniyya) pamoja na makao makuu ya Maahadi katika mkoa wa Najafu na tawi la Araak lililopo jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Kuhusu semina hizo tumeongea na mkuu wa Maahadi ya Quráni kitengo cha wanawake Ustadhat Manaar Jawaad Aljaburi, amesema kua: “Semina za Quráni kwa wasichana za kipindi cha majira ya joto ni moja ya miradi inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kutumia vizuri wakati wa likizo, na kuwajenga mabinti katika Quráni sambamba na kuwapa malezi mema ya kiislamu, kwani huenda pamoja na masomo ya Akhlaq na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) na Ahlulbait wake watakasifu (a.s), ikiwa ni sehemu ya kutengeneza kizazi chenye uwelewa wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Ratiba za masomo katika semina hizo zimeandaliwa na wasomi waliobobea katika Quráni na hukumu zake, pamoja na masomo ya Fiqhi, Aqida na Akhlaq, masomo yato yanafundishwa kwa kufuata umri wa washiriki, ambao umri wao ni kati ya (miaka 9 hadi 22), vilevile wanafundishwa na masomo ya kazi za mikono”.

Akabainisha kua: “Kwa ajili ya uhai wa mradi huu, Atabatu Abbasiyya imeandaa mahitaji yote muhimu kuanzia nakala za Quráni hadi usafiri, mwaka huu tumepata mwitikio mkubwa kutoka kwa washiriki ambao wameona umuhimu wa kuongeza uwezo wa kusoma Quráni na kutumia vizuri kipindi cha likizo za kiangazi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: