Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) katika kituo cha Al-Ameed Duwaliyyu Lilbuhuthi wa Dirasaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya nadwa yenye anuani isemayo: (Israiliyaat katika vitabu vya Siratu Nnabawiyyah.. utafiti wa kihistoria katika dalili na athari), mhadhiri wa nadwa hiyo alikua ni Dokta Karim ndani ya ukumbi wa mikutano wa kituo cha Al-Ameed, na kuhudhuriwa na wasomi bobezi wa historia kutoka vyuo vikuu mbalimbali.
Rais wa Daru Ustadh Aadil Nadhiir Biri amesema kua: “Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) inaangazia miradi ya kitafiti, miongoni mwa miradi hiyo ni kongamano la Siratu Nabawiyya, linalenga kuangalia vizuri historia na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) kwa namna ambayo inaendana na zama hizi, miongoni mwa majukumu ya Daru Rasuulul Aádham (s.a.w.w) ni kufanyia utafiti maudhui maalum, nadwa hii inanzungumzia moja ya jambo muhimu katika historia ya Mtume pamoja na Quráni tukufu, kwa kuangalia mambo ya Israiliyaat, hakika maudhui hii inaumuhimu mkubwa sana, Daru Rasuul Aádham imechagua Ustadhi aliye bobea katika mambo haya, pamoja na wasomi wengine wa sekula kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa Iraq, kwa ajili ya kujadili na kuchambua mada hii”.
Dokta Karim Mudhwahar mtoa mada wa nadwa hii amesema kua: “Nadwa hii ni miongoni mwa juhudi za Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) katika mradi wake mkubwa wa kusoma historia ya Mtume kwa kufuata muongozo wa Qur’ani tukufu, mada ya leo imechambua kwa kina jambo hilo, kuwepo kwa habari za Israiliyaat sio jambo geni katika historia, lakini linamitazamo mbalimbali, hakika jambo hilo lina athari kubwa katika vitabu vya historia ya Mtume (s.a.w.w), limejaribu kupunguza heshima ya Mtume (s.a.w.w) na zikataka kufuta utakasifu wake”.
Baada ya kumaliza kuwasilisha mada washiriki walipewa nafasi ya kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu mada hiyo, na mwisho kabisa wakapewa vyeti vya ushiriki na midani, kama sehemu ya kuonyesha kujali ushiriki wao na michango yao katika nadwa.