Maandalizi ya mapema ya kufanya kongamano la Ruhu Nubuwwah awamu ya nne

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya shule za Dini za Alkafeel za wasichana, na rais wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah ametangaza kuanza maandalizi ya kufanya kongamano hilo awamu ya nne, litakalo fanyika sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), linalo lenga kuelezea utukufu wa bibi huyo mtakatifu pamoja na mambo ya Dini, utamaduni na familia.

Akaongeza kua: “Maandalizi ya kongamamano yameanza mapema kwa kuandaa mada zitakazo wasilishwa pamoja na masharti ya ushiriki, pia yamejadiliwa mambo ya kiufundi yanayo endana na maendeleo ya sasa sambamba na kuchambua fikra za bibi Zaharaa (a.s)”.

Akasisitiza kua: “Kuna kazi nyingi zinazo fanywa na kamati inayo simamia kongamano, kwa ajili ya kuhakikisha kongamano linaendana na mwenye kuadhimishwa, ili uwe muendelezo wa mafanikio yaliyo patikana katika makongamano yaliyo pita”.

Kumbuka kua lengo la kufanywa kongamano hilo ni kubainisha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) na mchango wake katika uislamu kupitia mada za kitafiti zitakazo wasilishwa, pamoja na kuingiza vitabu vyake katika maktaba na kubaini turathi za mbora wa wanawake wa duniani (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: