Kitengo cha kusimamia nidhamu kinaendesha semina ya madhara ya dawa za kulevya na namna ya kujiepusha nazo

Maoni katika picha
Baada ya Marjaa Dini mkuu kutahadharisha katika khutuba ya Ijumaa kuhusu hatari ya kuenea kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana, kitengo cha kusimamia nidhamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutoa semina kwa watumishi za kuelezea madhara ya dawa za kulevya katika jamii, wanatoa mchango wao katika kuelimisha jamii madhara ya dawa hizo.

Semina hii imefanywa baada ya kuwasiliana na idara ya kupambana na dawa za kulevya ya mkoa wa Karbala kwa ajili ya kupata wakufunzi wa semina, mkuu wa idara ya kupambana na dawa za kulevya bwana Hussein Swadiq amesema kua: “Kutokana na maombi ya ndugu zetu watumishi wa kitengo cha kusimamia nidhamu katika Atabatu Abbasiyya na umuhimu wa kutoa mafunzo ya madhara ya dawa za kulevya zinazo haribu vijana wa Iraq, tumefanya semina ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) kuhusu dawa za kulevya na sababu za kuenea kwa biashara hiyo, sambamba na kuangalia mambo yanayo sababisha kuongezeka kwa idadi ya watumiaji, pamoja na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu namna ya kupambana na hatari hayo”.

Akaongeza kua: “Semina hiyo imefanywa kipindi muafaka kutokana na kuongezeka kwa changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana, inafanyika kwa muda wa siku nne, tunatarajia kufikisha ujumbe kwa wote kuhusu madhara ya dawa za kulevya ya sasa na ya baadae”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: