Wanajali kutoa huduma nzuri: Hospitali ya Alkafeel yaweka kifaa cha kisasa zaidi kwa ajili ya kupima mwili wa mwanadamu

Maoni katika picha
Kutokana na juhudi zake za kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kupitia vifaa vya kisasa kwa wananchi wa taifa hili, na kuweka mazingira bora ya kimatibabu, hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka kifaa cha kisasa zaidi hapa Iraq (Vo2 max) kwa ajili vipimo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Ahmad Swalehe Twayyaar: “Kifaa hiki ni muhimu sana katika hospitali hasa kwa wanamichezo na watu wote kwa ujumla na kinafanya kazi kielektronik”.

Akaongeza kua: “Kinapima kiasi cha Oksijeni katika mwili na namna inavyo tumika, pamoja na kubaini kiwango cha upumuaji sambamba na kupima uwezo wa moyo na mapafu, kwa kupata majibu ya vipimo hivyo unaweza kupanga vizuri ratiba ya mazowezi kulingana na uwezo wa muili wako”.

Mwisho akatoa wito kua: “Wanamichezo wote au mtu yeyote anayetaka kujua hali ya afya yake aje apime kupitia kifaa hiki, nacho hutumiwa sana na watu wa nchi zilizo endelea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: