Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike inaendelea na ratiba zake za wasichana katika majira ya kiangazi

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu lsemayo: (Hakika Hussein –a.s- ni taa la uongofu na safina ya uokozi) na msaada wa Atabatu Abbasiyya kwa kuandaa mazingira mazuri na kunyoosha mikono yake kuwapokea wanaharakati na kuwapa kila wanacho hitaji sambamba na kuwapa mafunzo ya kitamaduni na kimichezo, chini ya ratiba inayo endana na umri wa washiriki.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike chini ya kitengo cha maarifa ya kibinadamu na kiislamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na ratiba zake mbalimbali za kiangazi.

Makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike bibi Taghrida Tamimi amesema kua: “Wanafunzi tumewagawa makundi ishirini na moja kutokana na umri wao, tuna jumla ya wanafunzi (490), selebasi inamasomo ya mbalimbali yakiwemo masomo ya Fiqhi, Aqida, Quráni na Sira, pia wanafundishwa hati za kiarabu pamoja na lugha ya kiengereza na mbinu za kuhkutubu sambamba na kazi za mikono”.

Kumbuka kua semina za wasichana katika majira ya kiangazi ni miongoni mwa miradi muhimu inayo simamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ratiba bado inaendelea ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi, na imepata mwitikio mkubwa, Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa kila kitu kinacho hitajika kuanzia nakala za Quráni na vitabu vya Fiqhi na Aqida pamoja na usafiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: