Madrasa tofauti za Quráni zikiendesha visomo: Masomo yanaendelea katika semina za mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa

Maoni katika picha
Warsha za usomaji wa Quráni katika awamu ya tano ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa ambayo inajumla ya washiriki (120) ambao wamewekwa katika madrasa tano zilizo chini ya mradi huu.

Kwa mujibu wa maelezo ya msomaji Sayyid Hassanain Halo mkuu wa kituo cha miradi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya: “Mradi unafanywa kwa mwaka wa tano mfululizo ndani ya kipindi cha likizo za kiangazi, kwa lengo la kuandaa idadi kubwa ya wasomaji, na kuwafikisha katika kiwango kizuri kwa muda wa miezi miwili takriban kama sehemu ya kwanza ya mradi, walengwa wa mradi ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari”.

Akaongeza kua: “Mwaka huu tumepokea wanafunzi (120) walio timiza masharti ya kushiriki, tumewagawa katika madrasa tano, ambazo ni: (Madrasa ya Haafidh Khaliil Ismaili kwa mahadhi ya kiiraq, Madrasa ya Shekh Abdulfataah Sha’shaai, Madrasa ya Shekh Muhammad Swadiiq Minshawi, Madrasa ya Shekh Shahata Muhammad Anuur na Madrasa ya Shekh Abu Ainain Shaishai), kuna idara maalum ya watoto wa mashahidi na wapiganaji wa Hashdi Shaábi ambao ni miongoni mwa washiriki wapya waliokubaliwa, katika kipindi hiki wanafundishwa masomo mbalimbali”.

Akafafanua kua masomo haya yanaendelea kwa muda wa miezi miwili mfululizo katika jengo la Alqami chini ya Atabatu Abbasiyya, chini ya wakufunzi mahiri, kwa kufuata ratiba maalum yenye masomo ya hukumu za usomaji, sauti, naghma, kusimama, kuanza na adabu za kubeba Quráni, wanafundishwa kwa vitendo pia, pamoja na ratiba ya masomo ya kimalezi na kuna vipindi vya michezo na mapumziko ndani ya muda wote wa mradi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: