Jumuwiya ya Alkafeel ya Skaut imezindua ratiba ya kwanza ya awamu ya tatu, inayo husisha kikosi cha Aljawaalah vijana wenye umri wa miaka (16 – 18), kipengele cha kwanza kilikua ni kuwatambua washiriki, na mambo yote ya msingi katika Skaut kama vile salamu na mambo mengine, sambamba na mihadhara iliyo tolewa katika uwanja na bustani za jengo la Alqami ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kwa hamasa ileile kimefanywa kipengele cha pili kilicho husisha mchezo wa mpira wa miguu ulio fanyika ndani ya uwanja wa michezo wa jengo la Alqami, katika siku ya kwanza ya ratiba ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wanaskaut kwa awamu ya tatu.
Ratiba ya siku ya kwanza ikahitimishwa na kipengele cha kuogelea, ambapo walipelekwa kwenye bwawa la kuogelea ndani ya mji wa Karbala.