Watumishi wa utunzaji wa viatu katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kazi kubwa

Maoni katika picha
Watumishi wa utunzaji wa viatu chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kazi kubwa, kutokana na huduma wanazo toa kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanafanya kazi usiku na mchana.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Ahmadi Hashim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Idara ya utunzaji wa viatu ni miongoni mwa idara zinazo wahudumia mazuwaru moja kwa moja, kwa hiyo watumishi wake wanapambika na sifa nyingi kama vile, subira na bashasha, jumla ya watumishi wa idara hiyo ni (142), hupewa semina mbalimbali za kidini kwa ajili ya kuwajenga ili waweze kutoa huduma nzuri kwa mazuwaru, pamoja na kuwapa kozi za lugha tofauti ili waweze kuwasiliana na mazuwaru wa kigeni.

Akaongeza kua: “Tuna vituo ndani ya ukumbi mtukufu wa haram na kwenye kila mlango tuna sehemu za kutunzia viatu, pia tunamilango maalum kwa ajili ya wanawake peke yao, jumla ya vituo vya kutunzia viatu vipo (43) vya wanaume na wanawake kwenye milango yote ya Ataba tukufu”.

Akaendelea kusema: “Huwa tupo makini sana tunapotoa namba kwa zaairu, namba za kwenye kila kituo zinatofautiana rangi na namba za kituo kingine, ili kumrahisishia zaairu kutambua kwa urahisi sehemu alipo acha viatu vyake baada ya kumaliza ziara”.

Akasema: “Tunawafanya kazi wa kujitolea pia ambao huja kumtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka miji tofauti ya Iraq, hasa katika ziara kubwa na siku za Ijumaa kila wiki”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunafanya kazi saa (24) kila siku, hatuishii kutunza viatu peke yake bali tunatoa msaada kwa mazuwaru wenye umri mkubwa na wenye ulemavu wa kuwaingiza katika ukumbi wa haram na kuwawezesha kufanya ziara kwa kutumia tololi maalum”.

Fahamu kua kitengo cha utumishi kwa kupitia idara zake mbalimbali kinafanya kazi kubwa sana ya kuwahudumia mazuwaru wa mwezi wa bani Hashim (a.s) chini ya ratiba maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: