Kimebeba baina ya jarada mbili mada nyingi za aina mbalimbali: Jarida la (Turathi za Hilla) latoa chapisho la kumi na moja

Maoni katika picha
Katika mwendelezo wa machapisho yake, hivi karibuni kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa chapisho la kumi na moja la jarida la (turathi za Hilla) ambalo huandika taarifa za mji wa Hilla, nalo ni moja ya majarida yanayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Chapisho la kumi na moja linamada mbalimbali zilizo andikwa na wasomi kutoka vyuo vikuu mbalimbali, lina mada za kihistoria na kifiqhi pamoja na mambo yanayo husiana na uhakiki wa nakala kale za Hilla,

Mada hizo zimejikita matika mambo matatu makuu, ambayo ni:

Kwanza: Uhakiki, unamada mbili ambazo ni: (Risalatul I’tiqadi ya Sharafu Dini Abu Abdillahi bun Qassim Uudiy Alhilliy, na Ijaza ya Sayyid Qawamu Dini Qazwini, na Muhtasari wa Sayyid ibun Maásuum Almadani wa mwaka 1120h).

Pili: Kifungu maalum kuhusu Sayyid ibun Twausi katika tafiti tatu za kisekula ikiwemo: (khitwabu toshelezi ya mwaka 664h), vita ya kifikra na kiitikadi na mijadala ya ibun Twausi.

Tatu: Mada tofauti kulingana na milango ya jalida.

Pamoja na mambo mengine ya kielimu, nakala hiyo inapatikana katika vituo vya mauzo vilivyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika mkoa wa Karbala karibu na mlango wa Kibla katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: