Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel inaendelea na mafunzo ya awamu ya tatu

Maoni katika picha
Katika kuendeleza safari ya kujenga jamii ya watu wanao jitambua, jumuwiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa mafunzo ya awamu ya tatu, kwa vijana wa Skaut wenye umri wa miaka (13 hadi 15) wapatao (400).

Mafunzo ya kwanza yanahusu (vipengele vya Skaut), kwa ajili ya kuwafundisha mambo muhimu katika Skaut kwenye mafunzo haya ya awamu ya tatu, mihadhara ya mafunzo hayo imetolewa katika bustani za mji wa mazuwaru Alqami uliochini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ratiba ya pili ilikua ni mashindano ya mpira baina ya wahitimu wa awamu ya pili na hawa wanaosoma awamu ya tatu, mashindano hayo yamefanyika ndani ya kiwanja cha michezo katika jengo la Alqami kama moja ya ratiba ya burudani.

Kumbuka kua ratiba ya mafunzo ya Skaut (PDF) katika majira ya kiangazi inahatua tatu (Al-Ashbaalu, Alkashaafah na Aljawaalah) kuanzia vijana wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nane, wanasomeshwa mambo tofauti na kupewa mihadhara ya aina mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: