Maukibu ya kutoa misaada kutoka Bagdad yashiriki katika opresheni ya (Iradatu Nasri) pamoja na majemedari wa Hashdi Shaábi

Maoni katika picha
Muendelezo wa misafara ya awali katika mufanya utaratibu walio jiwekea tangu kutolewa kwa fatwa ya kujilinda, kwa kuwasaidia walioitikia fatwa hiyo tukufu, msafara wa Labaika yaa Iraq wa (Ukoo wa Sudani) ambao ni sehemu ya misafara ya wakazi wa Bagdad chini ya idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamekwenda kutoa misaada kwa wapiganaji wa kujitolea wa Hashdi Shaábi na wanajeshi wa serikali katika mkoa wa Nainawa mji wa Hadhar, kwa vikosi vinavyo shiriki katika oprosheni ya (Iradatu Nasri) iliyo anza hivi karibuni kwa ajili ya kupambana na mabaki ya magaidi wa Daesh.

Mkuu wa Msafara Shekh Tahsin Sudani amesema kua: “Ni utukufu kwetu kutoa misaada hii kwa ndugu zetu na watoto wetu wanajeshi wa serikali na Hashdi Shaábi, wakati wanaendelea kuvunja ngome za magaidi, tumekuja katika mji wa Hadhar ambao ni mji muhimu katika opresheni hii”.

Akaongeza kua: “Smafara huu umebeba aina tofauti za vyakula, akasisitiza: “Hakika tutaendelea kufanya misafara ya aina hii katika maeneo mbalimbali, hili ndio jambo dogo tunalo weza kuchangia kwa majemedari hawa”.

Wapiganaji walio tembelewa wameshukuru sana msafara huo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuendelea kuwasaidia bila kuchoka tangu vita ilipo anza hadi leo, wakasema kua misaada hiyo sio migeni kwa Atabatu Abbasiyya kwani imekua ikisaidia wapiganaji tangu ilipo tolewa fatwa ya kujilinda hadi leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: