Baada ya makubaliano na wamiliki wake: Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimeanza kuvunja nyumba zilizopo katika hatari ya kuanguka ndani ya mji wa Karbala

Maoni katika picha
Mji mkongwe wa Karbala unanyumba zilizo jengwa miaka mingi iliyo pita, kutokana na ukongwe wa nyumba hizo, baadhi yake hazina matengenezo yeyoto toka zijengwe na baadhi hazina watu wanao ishi ndani yake, jambo linalo pelekea kubomoka sehemu ya nyumba, huku asilimia kubwa ya nyumba hizo zikiwa katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru, ndipo wenyeji wa maeneo hayo wakaleta maombi rasmi kwa Ataba tukufu ya kuvunja nyumba hizo.

Baada ya kuongea na wamili wa myumba hizo kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kuvunja nyumba hizo.

Fahamu kua kwa mujibu wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi kazi zinafanywa kwa umakini mkubwa, kwa ajili ya kuhakikisha hazisababishi madhara kwa mtu yeyote baada ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi kufanya ukaguzi wa nyumba zinazo takiwa kubomolewa pamoja na kubaini njia zitakazo tumiwa na mazuwaru wakati kazi inaendelea bila kuwapa usumbufu wowote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: