Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa.

Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa Imamu Hussein siku ya (8 Dhulqaada 1440h) sawa na (12 Julai 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ameongea vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo gusa maisha halisi tunayo ishi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:




    • - Kila mtu hujifaharisha kwa utaifa wake, jambo hilo lipo pia hapa Iraq tunajifaharisha kwa mambo mengi mazuri katika taifa letu.




    • - Miongoni mwa utamaduni wa watu wa taifa hili ni kuishi kikoo.




    • - Koo za wairaq zinahistoria ndefu na muhimu pamoja na matukufu mengi.




    • - Malezi ya kikoo yanamafundisho mengi ya kimalezi.




    • - Kutokana na umuhimu wa ukoo unaweza kua sababu ya vurugu kwa mtu asiyelitakia mema taifa.




    • - Ukoo ni hazina muhimu na chanzo kikubwa cha elimu katika jamii.




    • - Hivi karibuni kuna baadhi ya mambo yameanza kujitokeza na kuharibu maadili ya familia.




    • - Jambo muhimu kwetu ni kuona mambo mazuri yanaendelea.




    • - Mkosaji anatakiwa apewe nasaha na sio kumsaidia katika makosa yake wala haitakiwi kumuadhibu zaidi ya kosa lake, kufanya hivyo sio sawa.




    • - Unaweza kuchukua haki yako na kulinda haki za wengine.




    • - Kuna njia za kurekebisha makosa, haifai kulipiza kosa kwa kufanya kosa.




    • - Taifa letu linawatu wenye busara lazima tutatue matatizo kwa umakini.




    • - Lazima tutumie njia zinazo kubalika, zisizo pingana na utamaduni wetu wala sheria.




    • - Ugaidi haukuwepo na kama ulikuwepo haukuonekana.




    • - Enyi vijana nyie ndio nguvu kazi msikate tamaa ya maisha yenu kwa tatizo moja au mawili.




    • - Enyi vijana msichukue mfano kwa mtu aliyefeli, aliye feli hafai kua mfano wako.




    • - Enyi vijana fateni nasaha kutoka kwa aliye faulu.




    • - Enyi vijana jifunzeni kuomba ushauri kutoka kwa watu wengine.




    • - Enyi vijana msiweke maisha yenu hatarini ugaidi ni jambo hatari.




    • - Ewe kijana ugaidi ni kazi ya walioshindwa.




    • - Ewe kijana ugaidi unatokana na uvivu wa kutafakari na uchache wa akili, na gaidi hukana maisha yake.




    • - Kujiuwa na kuacha msiba katika familia yako sio ushujaa.




    • - Enyi vijana msijifunze kutowajali watu wengine.




    • - Ewe kijana jivunie uwezo wako na ujiamini lakini kumbuka wewe sawa na nguzo unahitaji msingi yaani mtu wa kukuongoza na hilo sio dosari.




    • - Enyi vijana mpo katika umri bora msidanganike na baadhi ya mambo ukaharibu maisha yetu.




    • - Ewe kijana maisha yapo mbele yako lazima uwe imara, shujaa, ,mwenye subira.




    • - Mwanadamu anapotaka kitu hukipata.




    • - Enyi vijana nyie ni watoto wa wakina mama watukufu na wakina baba watakatifu.




    • - Gaidi ni mtu dhaifu aliye shindwa muoga wa maisha ndio maana huamua kufanya ugaidi kwa gharama ya maisha yake.




    • - Pambaneni katika maisha kwa ushujaa na nguvu, Mwenyezi Mungu mtukufu atakusaidieni kwa kukufungulieni mambo mengi.




    • - Maisha yanahitaji kuwa na muongozaji na mtu unaye mtegemea.




    • - Usifanye haraka kuondoa uhai wako kwa mambo ya kipuuzi sana.




    • - Enyi vijana sisi tunapenda na tunatamani kuwaona mkijenga taifa hili, kwa kufanya mambo mazuri na sio yale yasiyo faa.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: