Kitengo cha majengo ya shule katika idara ya malezi ya Karbala kinahitaji kufungua ushirikiano na Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mafanikio waliyo pata yamekua na matokeo mazuri kwa Ataba, Ataba inakaribisha ushirikiano na kila mtu, sawa uwe ushirikiano wa kimawazo au kiuzalishaji, ugeni kutoka kamati ya utafiti na maendeleo chini ya kitengo cha majengo ya shule katika mji wa Karbala umetembelea moja ya miradi muhimu ya ufyatuaji wa tofali kavu na nguzo.

Ziara hii inakusudia kufungua ushirikiano baina yao, wamepewa maelezo ya kiufundi na kihandisi pamoja na kuambiwa namna walivyo fanikiwa kuingia katika soko la Karbala.

Mwisho wa ziara wageni wakaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa nafasi ya kuja kutembelea mradi huu, kwa ajili ya kuangalia moja kwa moja utendaji wa mradi na mafanikio waliyo piga kupitia raia wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: