Maktaba ya chuo cha Al-Ameed imejaza tafiti za wanafunzi wa elimu ya juu kutoka nje ya Iraq katika kabati zake za vitabu

Maoni katika picha
kituo cha misingi ya kujifunza (maktaba kuu) katika chuo cha Al-Ameed pamoja na usasa wake lakini inafuata njia za kujiendeleza kwa kutumia uwezo na vipaji vya wanafunzi wa elimu ya juu, wao ndio kiungo cha kutengeneza maktaba ya kielimu inayo kidhi mahitaji ya mwanafunzi.

Mkuu wa kituo hicho Ustadh Wasim Twalib Mahadi amesema kua: “Miongoni mwa hatua zilizo fanywa na kituo kwa kushirikiana na mradi wa mafaili unao simamiwa na maktaba pamoja na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni kuchukua kazi (tafiti) za wanafuzi wa elimu ya juu wanaosoma nje ya Iraq kwa lengo la kunufaika nazo, hivi karibuni maktaba imepokea mzigo wa vitabu kutoka wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu ikiwa ni mara ya pili ya kupokea kazi (vitabu) hivyo na bado wataendelea kupokea vitabu vingine”.

Akasisitiza kua: “Kuna mizigo miwili itakayo pokelewa hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kutunza juhudi za kielimu zinazo fanywa na wanafunzi walio jitolea kufanya utafiti wa mambo mbalimbali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: