Miongoni mwa miradi ya kibinadamu inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu: kituo cha Ummul Banina (a.s) Alkhairiyya cha matibabu ya meno

Maoni katika picha
Kituo cha Ummul Banina (a.s) Alkhairiyya cha matibabu ya meno chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni kituo cha kitaalamu na cha kwanza hapa Iraq katika maswala ya kinga na tiba ya meno, kinatoa kipaombele zaidi kwa watoto wenye miaka (6 hadi 12) kinapokea wagonjwa wa aina zote kutoka mikoa tofauti, hususan mayatima na watu wanaotoka katika familia masikini, kwa kuwasiliana na taasisi pamoja na ofisi za Maraajii zilizopo katika miji husika, wamepokea mamia ya wagonjwa kutoka mkoa wa Karbala na wote wamepewa matibabu na kuwa chachu ya kuendelea katika mikoa mingine chini ya ratiba maalum.

Huu ni miongoni mwa miradi ya kibinadamu inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu unao lenga kutoa mahitaji ya lazima ya kimatibabu kwa watoto, lengo kuu la kituo hiki ni kutoa kinga ya maradhi ya meno kwa watoto pamoja na kutoa tiba kwa wagonjwa wa meno, wanapewa kitu maalum kinacho zuwia maradhi ya meno ambayo huwapata watu wengi.

Kituo kinatoa huduma bure, madaktari wanao endesha mradi huu ni madaktari bingwa na wanajitolea, wanafanya kazi kwa muda wa saa (7) kila siku, baadhi yao ni wairaq na wengine wametoka nje ya Iraq, Atabatu Abbasiyya tukufu imewapa makazi na usafiri pamoja na vifaa tiba.

Kumbuka kua kituo hiki kilichopo katika chuo kikuu cha Al-Ameed barabara ya (Najafu – Karbala) kimeanzishwa kutokana na kuhisi majumumu kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kunako sababishwa na utukufu wa mwenye malalo hii Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na uchache wa vituo vya matibabu ya meno, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaona umuhimu wa kufungua kituo maalum kwa ajili ya kutoa kinga na tiba ya maradhi ya meno kwa watoto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: