Kwa Ridhwa limechomoza jua la uongofu: Atabatu Abbasiyya tukufu imepambwa vazi la furaha kwa kuzaliwa Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Inafaa Dunia ipambike kwa vazi la furaha, kwa kuzaliwa Imamu Sultani wa Ahlulbait Abulhassan Ridhwa (a.s) Imamu wa nane na Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) aliyezikwa katika ardhi ya Tusi iliyo ahidiwa pepo kwa atakae mtembelea.

Kutokana na kusherehekea mazazi hayo yanayo sadifu Jumatatu (11 Dhulqaada 1440h) sawa na (15 Julai 2019m), mazingira ya furaha yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuadhimisha tukio hilo tukufu.

Kama kawaida katika kuadhimisha mazazi ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum, kutakua na hafla ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuweka mauwa kwenye milango ya malalo takatifu, na kuwasha taa za rangi pamoja na kupuliza marashi mazuri, hali kadhalika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu utashuhudia hafla nyingi na vikao vya usomaji wa mashairi.

Kumbuka kua Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) ni Imamu wa nane miongoni mwa Maimamu watakasifu, alishika Uimamu baada ya kifo cha baba yake Imamu Alkaadhim (a.s) na aliogoza kwa muda wa miaka (20), ana majina mengi ya laqabu, mashuhuri zaidi ni: Ridhwa, na kuniya yake ni Abulhassan wa pili, alizaliwa katika mji wa Madina mwaka wa (148h), akauwawa kwa sumu iliyo wekwa kwenye zabibu au kongamanga katika ardhi ya Tusi mwaka (203h), na akazikwa katika mji wa Mash-had, na kaburi lake lipo huko hadi leo hutembelewa na mamilioni ya watu kutoka nchi tofauti duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: