Kwa ajili ya kunufaika na watoto pamoja na kuibua uwezo wao na kulea vipaji walivyo navyo, kituo cha taaluma na kuendeleza vipaji Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa program kubwa ya watoto katika msimu wa kiangazi iliyo pewa jina la (masomo ya kiangazi) yanayo ratibiwa kwa kushirikiana na chama cha watoto wenye vipaji (IOT Kids).
Hii ni miongoni mwa program kubwa za kielimu na kimichezo katika msimu wa likizo za kiangazi hapa Karbala, mtoto atasoma mambo tofauti yatakayo msaidia kumjenga kiakili na kumuimarisha katika lugha ya kiengereza, masomo yote yanafundishwa kwa namna ya kuvutia inayo mshawishi mototo kujifunza.
Ustadh Samiri Swafi ambaye ni kiongozi wa kituo cha taaluma na kuendeleza vipaji Alkafeel ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kupitia program hii kitengo kimekusudia kutumia vizuri kipindi cha likizo za kiangazi kwa watoto, chuni ya maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeandaa kila kitu kinacho hitajika kwa ajili ya program hii kama vile kompyuta na vinginevyo, kila kitu tunafanya kwa kushirikiana na vitengo mbalimbali vya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaongeza kua: “Haya ni matokeo ya mafanikio yaliyo patikana katika program kama hizi zilizo pita, walengwa wetu wakuu ni watoto wenye vipaji (IOT Kids) ambao tunawafundisha namna ya kua na fikra chanya wakiwa katika mazingira mazuri yanayo tofautiana na mazingira ya shule, wanafundishwa pia namna ya kuandaa program na michezo ya kielekronik – program za roboti - vifaa vya kielekronik - program za kuongeza uwelewa kwa ujumla - kuogelea – jinsi ya kujilinda – safari za kielimu na kitalii – mashindano na michezo, na mengineyo”.