Imamu Ridhwa (a.s): Tunaangazia elimu yake katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Maoni katika picha
Mwezi kumi na moja Dhulqaada mikono huinuliwa mbinguni kumuomba Mola mtukufu, kutokana na kuzaliwa kwa Imamu mtakasifu (a.s) alete furaha kwa waumini kwani Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) alikua miongoni mwa waliofanya kazi kubwa ya kufundisha elimu na misingi ya kiislamu, alikua ni Imamu wa nne miongoni mwa Maimamu waliosaidiwa na mazingira kueneza mafundisho ya Dini kwa kiwango kikubwa, alikua bingwa wa elimu zote –kwa makubaliano wa wanahistoria- wameandika kua alikua na elimu kubwa zaidi kushinda watu wote wa zama zake, alikua bingwa wa hukumu za Dini, Falsafa, tiba na zinginezo.

Abuu Swalat Harawi ameongea elimu saba alizo kua nazo (a.s) na alikua mtu wake wa karibua, anasema: Sikupata kuona mjuzi zaidi ya Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), hakuna Aalimu yeyote aliye muona ispokua alishuhudia kama ninavyo shuhudia, Ma-amun aliitisha mkutano wa wasomi wa Dini, wasomi wa Fiqhi na sharia, wataalam wa masomo ya itikadi wakaweka mjala na Imamu (a.s) akawashinda wato, wote wakakubali utukufu wake na wakakiri kushindwa, hakika Imamu Ridhwa (a.s) alikua mjuzi zaidi kushinda watu wote wa zama zake, alikua Marjaa mkuu katika ulimwengu wa kiislamu, wanachuoni wote walikua wanakimbilia kwake pale wanapotatizwa na hukumu ya jambo lolote la kisheria na kifiqhi, alionyesha uwezo wake mkubwa katika mjadala wa Khurasani, Basra na Kufa, aliulizwa maswali magumu sana lakini aliyajibu kwa ufasaha wa hali ya juu.

Pia alikua na sifa nyingine (a.s), alikua mtaalamu wa lugha zote, hilo linathibitishwa na Abuu Ismail Sanadi anasema: Nilipokua India nilisikia kua Mwenyezi Mungu anamtu wa maajabu kwa waarabu, nikaondoka kwenda kumtafuta, nikaelekezwa kwa Ridhwa (a.s), nikamfuata nikiwa sijui kiarabu, nilipo kutana naye nikamsalimia kwa lugha ya Sanadiyya, akaniitikia kwa lugha yangu, nikaanza kuongea nae kwa lugha ya Sanadiyya na yeye ananijibu kwa lugha hiyohiyo, nikamwambia: Nilisikia kua Mwenyezi Mungu ana mtu wa maajabu kwa waarabu na mimi nimekuja kumtafuta, akasema (a.s): (Ni mimi). Kisha akaniambia (a.s): (uliza unacho taka). Nikamuuliza mambo mbalimbali akanijubu kwa ufasaha zaidi, kila aliye kutana na Imamu alithibitisha jambo hilo.

Haya ni machache katika mengi aliyokua nayo Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo uwawa na siku atakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: