Viongozi wa kijeshi (50) wamefanya kiapo cha kulitumikia taifa Adhuhuri ya leo Jumatatu (11 Dhulqaada 1440h) sawa na (15 Julai 2019m) baada ya kuapa ndani ya haram tukufu ya Abbasi katika kuadhimisha kuhitimu kwao mafunzo ya (ukufunzi wa askari maalum – ukufunzi wa askari wa muungano), kufanya hivi imekua desturi ya vyuo vingi vya kijeshi hapa Iraq, kwani Abulfadhil Abbasi (a.s) ni kielelezo cha kujitolea na ushujaa, na ndio sifa kubwa ya askari wa Iraq, vita waliyo pigana dhidi ya magaidi wa Daesh ni mfano wa wazi wa jambo hilo.
Kuhusu jambo hili tumeongea na Abdu Jawaad mmoja wa viongozi wa mafunzo hayo, amesema kua: “Leo tupo katika ugeni wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kujifunza kutoka kwao na kupata mazingatio, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutakua wanajeshi waaminifu katika kulitumikia taifa na raia wote, tunamuomba Mwenyezi Mungu adumishe neema ya amani na afya”.
Akaongeza kua: “Shukrani zetu za pekee ziwaendee Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mapokezi mazuri waliyo tupa, hakika wao ni msaada mkubwa kwetu na wametuhamasisha, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwezeshe sote kulitumikia taifa hili na raia wake”.
Kumbuka kua viongozi wa wanajeshi walio hitimu mafunzo walishirikiana na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kula kiapo ndani ya haram tukufu, baada ya kumaliza kula kiapo katika haram ya Imamu Hussein (a.s), kula kiapo mahala hapa huwajenga kiroho ukizingatia kua wamelelewa katika kufuata mwendo wa mwezi wa bani Hashim (a.s) kama unavyo simuliwa na historia.