Maoni katika picha
Herufi hizo zimeandikwa kwa hati ya (Thuluth Jalliy), ambayo ni moja ya hati halisi za kiiraq iliyo anzishwa katika zama za utawala wa bani Abbasi, zimeandikwa na mikono ya wairaq inayo watii na kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w).
Kumbuka kua dirisha la myweshaji wenye kiu Karbala (a.s) huzingatiwa kua dirisha lenye mapambo ya pekee, yaliyo tengenezwa kwa mikono ya wairaq wazalendo waliojitolea kumtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s).