Kitengo cha malezi na elimu ya juu chafanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wa idara ya maelekezo ya kididi tawi la wanawake

Maoni katika picha
Miongoni mwa semina zake za kuwajengea uwezo watumishi wa vitengo vya Ataba tukufu, kitengo cha malezi na elimu ya juu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya semina kuhusu athari na uwelewa wa kijamii kwa watumishi wa maelekezo ya kidini tawi la wanawake kwa muda wa saa (20).

Semina inamada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni: namna gani unaweza kupata matokeo chanya?, namna gani unaweza kuamsha hisia za nafsi za watu?, kanuni mashuhuri zenye athari kwa watu, mbinu za kuwasiliana na watu, namna gani unaweza kuchanganyika na watu na ukawaathiri?, watu muhimu wa kuwaathiri, ishi na watu kwa kiwango cha akili zao, hatari za watu walio athirika, athari kwa watawala na watawaliwa, utendaji wa kazi, uwelewa wa kijamii, maana ya uwelewa wa kijamii.

Makamo kiongozi wa kitengo tajwa Dokta Mushtaqu Muan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika mbinu za kuwasiliana na jamii ni jambo muhimu linalotakiwa kila anayefanya kazi ya kuelekeza watu azijue, kwa hiyo somo hilo ni miongoni mwa masomo tuliyo kusudia kuwafundisha dada zetu mubulighaat”.

Akaongeza kua: “Hili ni jambo muhimu katika sekta ya tabligh, tumeangalia mahitaji ya kuathiri na kuteka akili za wasikilizaji wakati wa kuwaelekeza kitu kwa kutumia vitendo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: