Idhaatul-Kafeel ya wanawake yarusha matangazo yake katika mji wa Bagdad na kuteka anga la mji mkuu

Maoni katika picha
Idhaatul-Kafeel ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu inasikika katika mji wa Bagdad kupitia mitabendi 98, baada ya kuweka nguzo katika ofisi za Idhaa zilizopo kwenye mji huo.

Kwa hiyo inasikika vizuri kabisa katika mkoa wa Bagdad pamoja na mikoa jirani, hatua hii tukufu inalenga kuwafikia wanawake wa mkoa wa Bagdad na kuwawezesha kutoa ujuzu walio nao ukizingatia kauli mbiu ya idhaa hii ni sauti ya mwanamke wa kiislamu.

Fahamu kua Idhaatul-Kafeel ilikua imesha anza kurusha matangazo yake katika mkoa wa Baabil na miji ya pembezoni mwake, hii yote ni katika jitihada za kupanua wigo wake na kuhakikisha tunamfikia mwanamke wa kiislamu popote alipo kupitia mita bendi (FM 101.9) baada ya kufika katika mikoa mingi ya Iraq.

Idhaatu-Kafeel inatofauti kubwa na idhaa zingine za Iraq na duniani kwa ujumla, watendaji na viongozi wote ni wanawake, wanawasilisha sauti ya mwanamke wa kiislamu kutokea ndani ya jengo tukufu la Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: