Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaimarisha usalama katika barabara inayo tumiwa na mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kimeimarisha usalama katika barabara inayotumiwa na mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika eneo lenye (km 200) hadi sehemu ya mpakani Urúr kama sehemu ya kutekeleza wajibu wake wa kiulinzi na kiutumishi kwa kushirikiana na viongozi wa opresheni za usalama.

Wamefanya hivyo baada ya kuombwa kuweka ulinzi katika barabara hiyo na viongozi wa jeshi la serikali, kwani kikosi kina uwezo na vifaa vya kutosha kuimarisha usalama katika jangwa hilo.

Taarifa kutoka kwa kamanda wa Liwaa ya Ummul Banina (a.s) Najmu Abdillahi Ali inasema kua: “Mwaka huu kikosi kimetumia mbinu za kisasa katika kuimalisha ulinzi, kimeweka vituo vya ukaguzi umbali wa (km 50), pamoja na kuweka ulinzi wa moja kwa moja barabarani kwa ajili ya kuwahakikishia usalama zaidi mahujaji”.

Akasema kua: “Kuna kazi ambayo vinashirikiana vitengo vyote vya kikosi pamoja na kutoa huduma mbalimbali kupitia mawakibu Husseiniyya, ikiwemo maukibu ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji”.

Akaongeza kua: “Kiongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) Shekh Maitham Zaidi na wasaidizi wake wanashiriki moja kwa moja utendaji pamoja na kusimamia harakati za wapiganaji pamoja na mambo ya mahujaji watukufu”.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinasimamia ulinzi wa barabara hiyo kwa mwaka wa tano mfululizo, na haujawahi kutokea uvunjifu wa amani ndani ya miaka yote hiyo, fahamu kua kifaru cha Alkafeel kinashiriki katika zowezi hili ikiwa ni kazi yake ya kwanza tangu kizinduliwe na kikosi hicho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: